TUNAJIVUNIA UTALII..TUULINDE...TUUTANGAZE..TURITHISHE VIZAZI VYETU

Thursday, August 1, 2019

ISIMILA, IRINGA, TANZANIA

Isimila ni eneo la kihistoria lililopo mkoani Iringa nchini Tanzania, katika kijiji cha Ugwachanya kwenye kata ya Mseke kilichopo kilomita 20 kutoka Iringa mjini karibu na barabara kuu ya A 104 kuelekea Mbeya. Njia ya kuingia si rahisi kuikuta: ukitokea Iringa iko kabla ya kufikia Tanangozi, upande wa kushoto. Eneo hili ni kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa wa Iringa. Bonde la Isimila lilikaliwa na watu tangu Zama za Mawe za Kale. Ni katika eneo hilo ndipo zana za mawe za kale na nguzo za asili za Isimila zilipogunduliwa tangu mwaka 1951. Zana hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka laki tatu hadi nne kabla ya Kristo. Miongoni mwa zana zilizopo katika korongo la Isimila, ambalo lina mikondo miwili, ni pamoja na mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe ya kombeo kwa ajili ya uwindaji. Korongo la pembeni lina mmomonyoko wa ardhi ulioacha nguzo za ajabu. Pia vifaa kama nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zana nyingine na shoka zilizotumika kwa kazi ya kuvunja mifupa, nyembe na visu. Pia ndani ya eneo hili mafuvu na mifupa mingi ilionekana; kati yake ilipatikana mifupa ambayo ilifanana na ya twiga wa hivi sasa, ila tofauti ni kwamba, mifupa hiyo iliashiria kuwa twiga hao walikuwa na shingo fupi, ambapo pia kulikuwa na aina tofauti ya viboko.

No comments:

Post a Comment

MFAHAMU CHIFU WA WAHEHE.....SHUJAA ALIYEPIGANA NA WAJERUMANI

Mkwawa au kwa jina refu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (1855 – 19 Julai 1898) alikuwa mtemi na kiongozi mkuu wa kabila la Wahehe katika T...