TUNAJIVUNIA UTALII..TUULINDE...TUUTANGAZE..TURITHISHE VIZAZI VYETU

Thursday, August 1, 2019

MFAHAMU CHIFU WA WAHEHE.....SHUJAA ALIYEPIGANA NA WAJERUMANI

Mkwawa au kwa jina refu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (1855 – 19 Julai 1898) alikuwa mtemi na kiongozi mkuu wa kabila la Wahehe katika Tanzania ya leo wakati wa upanuzi wa ukoloni wa Ujerumani mwishoni mwa karne ya 19. Tangu mwaka 1885 hivi Wajerumani walianza kuunda koloni lao katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (Tanganyika pamoja na Rwanda na Burundi za leo). Kwa njia za mikataba na Uingereza, Dola la Kongo (wakati ule mfalme wa Ubelgiji) na Ureno walio kuwa wakoloni wa maeneo jirani walihakikisha kwamba hao hawataingilia katika sehemu walizolenga. Mwaka 1888/1889 utawala wao ulitikiswa na vita ya Abushiri lakini baada ya kushinda upinzani wa Waafrika wa pwani Wajerumani walilenga kuimarisha utawala wao juu ya sehemu za bara. Mkwawa aliwahi kusikia mapema habari za Wajerumani akajaribu kuwasiliana nao lakini bila kuelewana. Hapo aliamua kujenga boma imara lenye kuta za mawe kwenye makao makuu yake huko Kalenga karibu na Iringa ya leo[1]. Katika mwezi Februari 1891 alituma wajumbe kwa kambi la Wajerumani huko Mpwawa wakapokewa na gavana Mjerumani. Wakati huohuo Mkwawa aliendelea kutuma askari zake hadi Usagara iliyotazamwa na Wajerumani kama eneo lao. [2] Katika kipindi hicho gavana mpya Julius von Soden alifika Dar es Salaam. Hakuwa na mamlaka juu ya mkuu mpya wa jeshi Emil von Zelewski aliyepokea amri zake kutoka Berlin moja kwa moja. Baada ya kusikia habari za mashambulio ya Mkwawa katika Usagara aliomba kibali cha "kuwaadhibu Wahehe" akakubaliwa.

ISIMILA, IRINGA, TANZANIA

Isimila ni eneo la kihistoria lililopo mkoani Iringa nchini Tanzania, katika kijiji cha Ugwachanya kwenye kata ya Mseke kilichopo kilomita 20 kutoka Iringa mjini karibu na barabara kuu ya A 104 kuelekea Mbeya. Njia ya kuingia si rahisi kuikuta: ukitokea Iringa iko kabla ya kufikia Tanangozi, upande wa kushoto. Eneo hili ni kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa wa Iringa. Bonde la Isimila lilikaliwa na watu tangu Zama za Mawe za Kale. Ni katika eneo hilo ndipo zana za mawe za kale na nguzo za asili za Isimila zilipogunduliwa tangu mwaka 1951. Zana hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka laki tatu hadi nne kabla ya Kristo. Miongoni mwa zana zilizopo katika korongo la Isimila, ambalo lina mikondo miwili, ni pamoja na mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe ya kombeo kwa ajili ya uwindaji. Korongo la pembeni lina mmomonyoko wa ardhi ulioacha nguzo za ajabu. Pia vifaa kama nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zana nyingine na shoka zilizotumika kwa kazi ya kuvunja mifupa, nyembe na visu. Pia ndani ya eneo hili mafuvu na mifupa mingi ilionekana; kati yake ilipatikana mifupa ambayo ilifanana na ya twiga wa hivi sasa, ila tofauti ni kwamba, mifupa hiyo iliashiria kuwa twiga hao walikuwa na shingo fupi, ambapo pia kulikuwa na aina tofauti ya viboko.

MFAHAMU CHIFU WA WAHEHE.....SHUJAA ALIYEPIGANA NA WAJERUMANI

Mkwawa au kwa jina refu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (1855 – 19 Julai 1898) alikuwa mtemi na kiongozi mkuu wa kabila la Wahehe katika T...